×

Mahakama Yawachia Huru Washtakiwa Watano Akiwamo Mkurugenzi wa Udart, Kisena

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewachia huru washtakiwa watano akiwamo Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka (Udart), Robert Kisena waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka 15 likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2 bilioni.

 

Mahakama hiyo imewaachi huru washtakiwa hao leo Ijumaa Juni 3, 2022 chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (PA) Sura ya 20 iliyofanywa marekebisho mwaka 2019 baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea kesi hiyo.

YANGA WATANGAZA UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI WAPYA, CEO SENZO, MCHUNGAHELA WAZUNGUMZA..

Leave a Comment