
WAKATI leo Juni 9,2021 ikiwa ni siku ya mwisho ya kurejesha fomu na kesho mchujo kuweza kuanza leo Injinia Hersi Said amerejesha fomu yake ya kugombea Urais wa Yanga.
Injinia amewakilishwa na wazee wa Yanga pamoja na Fredrick Mwakalebela ambaye rasmi amesema kuwa yeye hatogombea na kuwaaga wana Yanga kwenye nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi jana alichukuliwa fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Julai na wazee wa klabu hiyo.
Leo wazee wa Klabu ya Yanga wamerudisha fomu hiyo ikiwa imejazwa tayari kwa kuanza mbio za Urais wa Klabu hiyo.
Mwakalebela amesema kuwa Yanga wanatambua namna Injinia alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.