
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji wa Kyaka-Bunazi mkoani Kagera leo Juni 9, 2022 wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Rais Samia amesema mradi huo umejengwa kwa gharama za ndani na umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na utanufaisha Zaidi ya watu 65,470 wa Kata ya Kyaka na Kasambya pamoja na Vitongoji vyake.
Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi pamoja na wahandisi wa mradi huo ambao wengi wao wamefanya sehemu ya pili ya mradi.

Aidha Rais Samia ametoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhakikisha anazikopesha Mamlaka za Maji za Mkoa huo kuwakopesha kiasi cha Shilingi Milioni 500 ili ziweze kutekeleza miundombinu ya maji kwa wananchi kwa haraka.