×

Rais Samia: Nimevutiwa Sana na Ajira Niliyoikuta Hapa Kiwanda cha Sukari – (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema amevutiwa sana na kiwango cha ajira kilichotolewa na Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar).

 

Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwahutubia wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa ziara yake kiwandani ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera.

 

Rais Samia akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa kuzalisha Umeme Megawati 20 katika Kiwanda cha Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.  Rais Samia anaendelea na ziara yake Mkoani humo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.

 

“Nimekuta vijana wetu waliohitimu vyuo mbalimbali wako hapa wanafanya kazi hapa, wanaeleza mambo makubwa na nimewashuhudia wakifanya mambo ambayo huko nyuma kiwanda hiki kingehitaji wataalam kutoka nje kuja kuelezea namna ya kufanya lakini leo yanafanywa hapa.”alisema Rais Samia

Rais Samia, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mtambo wa kuzalisha Umeme Megawati 20 katika Kiwanda Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Rais Samia anaendelea na ziara yake ambayo ni siku ya pili Mkoani Kagera kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.

 

Aidha Rais Samia amesema kuwa ziara yake kwenye kiwanda hicho imekuwa na manufaa sana kwani ameweza kuona mwenyewe kwa macho yake changamoto alizokuwa akiambiwa ambazo awali alihisi kuwa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho alikuwa akilalamika tu.

Rais Samia akikata utepe kuzindua rasmi Vitendea kazi vya uendelezaji wa kilimo katika Mashamba ya Miwa yaliyopo kwenye Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.

 

Rais Samia pia ametumia fursa hiyo kuipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda pamoja na Wafanyakazi wote wa Kiwanda hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia amebainisha kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alimdokeza kuwa sekta ya sukari inaonesha mfano mzuri wa ukuaji mwaka hadi mwaka.

Rais Samia akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanroad Mhandisi Rogatus Mativila kuhusu kukamilika kwa Daraja la Kitengule linalounganisha Wilaya ya Misenyi na Karagwe Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Rais Samia anaendelea na ziara yake ya siku ya pili Mkoani Kagera kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Kwa upande mwingine Rais Samia amebainisha kuwa Serikali imetenga kiasi cha Bilioni 20 kwa ajili ya kuendeleza mashamba makubwa ikiwemo ya Miwa, Michikichi pamoja na Arizeti.

Leave a Comment