×

Mabadiliko Makubwa Kufanyika Ndani ya Konde Music Worldwide Maarufu kama Konde Gang

Mwijaku Mwemba (DC wa Insta)

Mwijaku; ni muigizaji na mtangazaji maarufu nchini Tanzania ambaye amefichua kuwa, kitendo cha Kajala Masanja kutangazwa kuwa CEO mpya wa timu ya usimamizi ya Konde Music Worldwide, kinakwenda kuleta mabadiliko makubwa ndani ya lebo hiyo.

 

Mwijaku anasema kuwa, Kajala ana uwezo mkubwa wa kuifanya Konde Gang kuwa bora zaidi.

 

Anasema kuwa muigizaji huyo anastahili wadhfa aliopatiwa na Harmonize kwa historia yake katika tasnia ya burudani Tanzania kwani ni ya kuvutia.

 

“Kajala anaingia pale kuongeza thamani. Ana utofauti mkubwa na wanawake wengine. Anakwenda kuchora njia Konde Gang kwenda kimataifa zaidi,” anasema Mwijaku.

 

Mwijaku anadokeza kuwa, kuna mabadiliko mengi mazuri katika Konde Gang katika muda wa miezi sita ijayo.

 

Anatoa hakikisho kuwa mpenzi huyo wa Harmonize ataleta utaratibu, uwajibikaji na urasimu ndani ya Konde Gang akihudumu kama CEO.

“Tumpe Kajala miezi sita, Konde G

ang itakuwa hatua ya juu zaidi katika tasnia ya burudani,” anasema Mwijaku.

 

Mwijaku pia anaweka wazi kuwa uhusiano wa kimapenzi kati ya Harmonize na Kajala hautaathiri utenda kazi wao.

Mapema wiki hii Harmonize alimteua Kajala kuwa meneja wake na CEO wa timu ya manejimenti ya Konde Music Worldwide baada ya kuzika ugomvi.

Kajala Masanja(Meneja wa Msanii Harmonize)

Meneja wake wa usanii, Choppa ndiye aliyetangaza habari za uteuzi wa Kajala huku akimkaribisha kwenye  timu yao.

“Niruhusu nimkaribishe katika timu ya usimamizi mkurugenzi na meneja mpya Frida Kajala. Nimefurahi kufanya kazi na wewe shem,” alitangaza Choppa.

 

Kajala anaungana na Chopa, Mjerumani na Jose Wamipango katika timu ya usimamizi wa Harmonize na Konde Gang Music Worldwide kwa jumla.

Leave a Comment