×

Madaktari Wapandishwa Kizimbani Kujibu Shutuma za Kifo cha Maradona

Gwiji wa soka duniani Diego Armando Maradona

JUMLA ya madaktari nane wanatarajiwa kupanda kizimbani kujibu tuhuma za kusababisha kifo cha gwiji wa soka duniani Diego Armando Maradona kutokana na kile kinachosemekana na uzembe na kushindwa kuwajibika.

 

Maradona alifariki mwezi Novemba 2020 kwa tatizo la shambulio la moyo katika mji mkuu wa Argentina Buenos Aires, akiwa na umri wa miaka 60.

 

Alikuwa akijiuguza nyumbani kwa muda wa mwezi mmoja ikiwa ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa baada ya damu kuvujia katika ubongo.

 

Siku chache baada ya kifo chake wanasheria walifungua kesi dhidi ya madaktari na wauguzi kwa ujumla kufuuatia kifo cha nguli huyo wa soka duniani.

Maradona anatajwa kuwa moja ya wachezaji bora wa mpira wa miguu wa muda wote

Mwaka jana iliundwa timu ya wataalamu 20 ambao walifanya kazi ya uchunguzi na kubaini kuwa madaktari na manesi waliohusika katika kutoa huduma kwa Maradona hawakuwa makini na walifanya kazi zao kwa uzembe jambo lililosababisha kifo cha gwiji huyo.

 

Ripoti ya utafiti huo ilibainisha kuwa Maradona angekuwa na nafasi kubwa ya kupona kama tu angeweza kuhudumiwa vizuri na kwa maadili.

 

Kama wakikutwa na hatia hukumu yao inaweza kuwa kati ya miaka 8-25 jela hiyo ni kwa mujibu wa sharia za makosa ya jinai ya nchini Argentina.

Leave a Comment