×

Bunge la Ulaya Laipigia Kura Ukraine na Moldova Kujiunga na EU

Bunge la Umoja wa Ulaya

UMOJA wa Ulaya EU leo umeipigia kura nchi ya Ukraine pamoja na Moldova kuzipatia hadhi ya ugombea wa kujiunga na umoja huo.

 

Kwa mujibu wa sheria za umoja wa Ulaya ni kwamba ili nchi iwe mwanachama wa umoja huo kwanza inahitaji kupata kibali cha kuwa mgombea ili iweze kupata nafasi ya kuchunguzwa na kutimiza matakwa ma vigezo vya kujiunga na umoja huo.

Kura zimepigwa katika Bunge lililokaa jijini Brussels Ubelgiji

Katika mkutano huo uliofanyika leo Jijini Brussels Ubelgiji umeshuhudia jumla ya kura 529 zikikubali Ukraine na Moldova kujiunga na Umoja huo huku kura 45 zikikataa.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Bunge la Umoja wa Ulaya ni kwamba linadhamiria kufanya hivyo pia kwa nchi ya Georgia mara tu baada ya nchi hiyo kutekeleza matakwa ya vigezo vya kujiunga na umoja huo.

Georgia nayo ipo katika harakati za kupatiwa kibali cha mapendekezo ya kujiunga na umoja wa Ulaya

“Watu wa Ukraine, Moldova pamoja na Georgia wanastahili kuishi kwa Amani na uhuru, demokrasia pamoja na maendeleo kwa nchi zao ambazo zitakuwa zikijisikia fahari kuwa sehemu ya jumuiya ya umoja wa Ulaya.

 

Kutokana na uamzui huo inasubiriwa kuona Urusi itachukua hatua gani kwani kwa muda mrefu imekuwa ikizitahadharisha nchi hizo ikiwemo pia Sweden na Finland kuhusu mpango wao wa kujiunga na umoja wa Ulaya ambao Urusi yeye anautazama kama hatari kwa usalama wan chi yake.

Leave a Comment