
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amewataka Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoa mawazo mazuri hata pindi wanapofikia ukomo wa utumishi wao ndani ya Jeshi.
Ametoa rai hiyo leo Juni 28 2022, wakati akifungua Jengo la kitega uchumi la Suma JKT jijini Dodoma lililogharimu Kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotokana na kukusanya faida baada ya kujenga miradi mbalimbali kama Wakandarasi.

Sambamba na hilo Jenerali Mabeyo ameyashukuru Mashirika mbalimbali yaliyotoa ushirikiano kwenye kufanikisha ujenzi wa Jengo hilo kama vile Tanesco na Tanroads huku akizihakikishia taasisi hizo kuwa Jeshi litatoa ushirikiano wa dhati kwa taasisi hizo.
Jengo hilo linaweza kutumika kwa ajili ya Ofisi mbalimbali za Serikali lakini pia shughuli za kibenki ili kuwarahisishia wananchi huduma kwani uhitaji bado ni mkubwa,
Jenerali Mabeyo anaelekea kumaliza muda wake wa utumishi.