×

Rais Samia Apongeza Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto CCBRT- Msasani Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada na ubora wa ujenzi wa jingo la Mama na Mtoto la CCBRT lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam katika halfla ya uzinduzi wake ambapo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

 

Rais Samia amesema ameridhishwa na kufrahishwa na ubora wa jingo hilo lakini pia huduma mbalimbali zinazotolewa katika jingo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa zitasaidia kuwasaidia wanawake kujifungua salama.

 

Akiongea na wananchi katika uzinduzi wa jingo hilo ambalo limepewa jina la Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amefurahishwa jingo hilo kupewa jina lake kwani alipopata fursa ya kutembelea na kujionea ustadi pamoja na ubora wake hakujutia jingo hata kidogo.

Rais Samia amepongeza ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto la CCBRT lililopo Mikocheni Jijini Dar es salaam

Aidha Rais Samia amesema malengo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5 wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni kupunguza vifo kutoka 321 kwa kila vizazi 100000 hadi kufikia vifo 220 kwa vizazi 100000 na mpango huo ni hadi kufikia mwaka 2025/2026.

 

Vilevile mpango huo umepanga kupunguza vifo vya watoto kutoka vifo 51 kwa kila vizazi hai 1000 hadi vifo 40 kwa kila vizazi hai 1000 na hiyo pia ni hadi kufikia 2025/2026.

 

Gharama za ujenzi wa jengo hilo zinakadiriwa kufikia kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 45 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 101 za Kitanzania.

Leave a Comment