×

Mbosso Afichua Bifu Lake na Aslay, Ataja Kilichoiua Yamoto Band

 

                                             Msanii wa Bongo Fleva Aslay

MBOSSO Khan; ni staa mkubwa wa Bongo Fleva ambaye amefichua kuhusu bifu lake la moto na memba mwenzake wa zamani wa Yamoto Band, Aslay huku akitupilia mbali madai kuwa chanzo cha tatizo lao ni wanawawake.

 

Mbosso anasema kuwa, hakuna sababu za msingi zilizosababisha ugomvi kati yao anasema kuwa, urafiki wao ulikatika ghafla tu baada ya Aslay kum-unfollow kwenye mitandao ya kijamii.

 

“Hakuna hata suala la maana ni upuuzi tu! Kitu gani cha maana hapo tulichogombania ni upuuzi tu kwamba huyu anafanya kazi zake huku na mwingine anafanya kazi zake huko, ghafla huyo wa huku kakunja na huyo wa huko kaona basi ikakuwa hivyo,” anasema Mbosso.

 

Mbosso anasema Aslay ndiye aliyetangulia kujitenga na Yamoto Band ili kuangazia kazi zake pekee yake baadaye, wanabendi wengine; Enock Bella, Beka Flavour na yeye, walitengana na kila mmoja akaanza kufanya kazi kivyake.

 

“Aliondoka akaamua kufanya maisha yake akatuacha sisi watatu tunaishi pamoja. Yeye alikuwa na mambo yake, alikuwa anatoa mangoma na sisi wengine tulikuwa tunamsapoti, sisi wengine hatukuwa na mangoma tulikuwa tunamsapoti kwa nafasi yake,” anasema Mbosso.

 

Mbosso anasema kuwa tofauti zake na mwenzake huyo wa zamani zilianza muda mfupi baada yake kujiunga na Lebo ya WCB iliyo chini ya Diamond Platnumz.

 

Hata hivyo, Mbosso anakana kuwa Aslay alimuonea kijicho kwa kuwa alianza kufanya vizuri Mbosso anapuulizia mbali madai kuwa kuna tofauti zilizopo kati yake na Beka Flavour ambaye pia alikuwa katika Yamoto Band anasema kuwa, anatamani sana tofauti zilizopo baina yake na wanabendi wenzake wa zamani wa Yamoto Band yaishe.

Leave a Comment