×

Uwoya Aibua Mshtuko Mgeni Rasmi Kanisani, Mchungaji Amchambua Kipekee

Irene Uwoya alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 8 ya kanisa la ufunuo Morogoro

IRENE UWOYA; ni mwanamama wa Bongo Movies ambaye ameibua mshtuko miongoni mwa wanajamii ya mitandaoni baada ya mhubiri mmoja nchini Tanzania kumualika kama mgeni rasmi katika sherehe za miaka 8 tangu kuanzishwa kwa kanisa lake.

 

Mchungaji aitwaye Bishop Geography Bendera alitangaza kwamba wanawake ni jeshi kubwa hivyo jana Jumapili kanisa lake la Ufunuo la mkoani Morogoro lilikuwa na ibada maalum kusherehekea wanawake.

Uwoya akiwa kanisani

“Wamama ni jeshi kubwa, Jumapili hii mama wa Ufunuo Morogoro, wana jambo lao, wakiwa na mwanamama mchapakazi, mjasiriamali, superwomen Irene Uwoya kama mgeni rasmi,” alisema Askofu Bendera.

 

Askofu huyo alisema Uwoya ni mwanamke anayejitegemea na mwenye uchumi imara.

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment