
MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Jembe kupitia kipindi cha Krosi Dongo amebainisha wasiwasi wake juu ya ukaribu na urafiki alionao Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na Makamu Mwenyekiti Arafat Haji.
Jembe amesema kuwa Injinia Hersi ana uzoefu mzuri na anaweza kuisaidia Yanga kufikia mafanikio yanayotarajiwa lakini ukaribu alionao na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Arafat Haji unaweza kusababisha asifanikishe malengo kwa wakati kwani itamuwia vigumu sana Arafat kumkosoa Injinia Hersi pale anapokosea.
Jembe amenukuliwa akisema:

“Hersi Capacity yake ni kubwa kuliko Arafat kwahiyo angekuwepo mtu mwingine ambaye anaweza kumuambia nje ya ushikaji, nje ya mazoea, nje ya kufahamiana akiwa serious anamuambia President No, President hapa tunakosea na kwa nilivyomsikiliza yule dada (Suma Mwaitenda) kwa hizi siku chache hakika naamini angekuwa msaada mkubwa sana.”

Tayari kupitia uchaguzi wa Julai 9, 2022 Injinia Hersi Said alifanikiwa kushinda nafasi ya Urais wa klabu ya Yanga huku Arafat Haji akiwa Makamu wa Rais wa Klabu hiyo.