×

Ahukumiwa kwa Kesi ya Kumbaka Mtoto wa Miaka 10, Ambaye alikataliwa Kutoa Ujauzito

Gershon Fuentes

MWANAUME mmoja katika mji wa Ohio nchini Marekani amehukumiwa kwa kosa la ubakaji baada ya kumpatia ujauzito binti mwenye umri wa miaka 10 ambaye alikataliwa kutolewa ujauzito wake.

 

Gershon Fuentes (27) amepelekwa Mahakamani katika Jimbo la Columbus, kujibu tuhuma hizo huku jina la binti huyo aliyepewa ujauzito limehifadhiwa kwa ajili ya taratibu za kiusalama.

 

Tayari Rais wa Marekani Joe Biden ameonesha kutokuridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo kufuta sharia inayoruhusu utoaji mimba kwa wanawake nchini humo.

 

Awali wanawake nchini Marekani walikuwa wanalindwa na sheria iliyokuwa inawapa uhuru wa kutoa ujauzito kulingana na sababu za masingi zinazolazimisha kufanyika kwa jambo hilo.

Mtoto ana ujauzito wa miezi sita (6) na siku tatu (3)

Kwa mujibu wa Gazeti la Indianapolis, motto huyo alikuwa na ujauzito wa miezi 6 na siku 3.

 

Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka motto huyo anasadikika kuwa alikuwa na umri wa miaka 9 wakati anapewa ujauzito huo

Leave a Comment