
Tiwa Savage; ni staa wa kike wa muziki nchini Nigeria ambaye ametunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Kent nchini Uingereza, Tiwa amepewa heshima hiyo kutokana na ushawishi katika tasnia ya muziki Chuo Kikuu cha Kent kilimuorodhesha Tiwa na mastaa wengine wengi kuwania shahada hiyo ya heshima.
Tiwa na Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Mwaka 2021 ya Fasihi, Abdulrazak Gurnah walikuwa miongoni mwa wahitimu wa heshima wa chuo hicho, Julai 2022.
Kabla ya heshima hiyo, awali Tiwa alipata shahada yake ya kwanza ya masomo ya Biashara kutoka Chuo Kikuu miaka kadhaa iliyopita na baadaye akapata ufadhili wa wa kusoma muziki wa kitaalam katika Chuo cha Muziki cha Berklee huko Boston, Massachusetts nchini Marekani.