
KATIKA moja ya Mgahawa Kusini-Magharibi mwa nchi ya China umegundulika unyayo wa Dinosaur anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni mia moja.
Ni katika Mgahawa uliopo katika Jimbo la Leshan, Sichuan nchini China ambapo zimegundulika nyayo za Dinosaur wawili aina ya Sauropods ambao wameishi kwa zaidi ya miaka milioni 100 iliyopita.

Mwana Akiolojia Lida Xing ambaye ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Nchini China (China University) yeye pamoja na timu yake walithibitisha kugundua nyayo hizo kwa kutumia teknolojia ya 3D Scanner.
“Ingawa mafuvu mengi ya Dinosaurs ya enzi za Jurassic yamegunduliwa hapa Sichuan, lakini ni mafuvu machache sana yamegundulika katika kipindi cha Mesozoic, hii ni sawa na kipande cha kukamilisha fumbo kwani inaongeza ushahidi kwa kuwepo na aina mbalimbali za Dinosaurs.” Alisema Xing.

Imebainika kuwa kabla ya kuwa Mgahawa eneo hilo lilikuwa likitumika kama shamba la kufugia Kuku ambapo nyayo hizo za Dinosaurs zilifukiwa na vumbi pamoja na mchanga ambao ulisaidia kuzikinga kupotea kwa mmomonyoko wa udongo pamoja na mabadilio ya hali ya hewa.