×

Barcelona Yamfungia Kazi Azpilicueta, Chelsea Yaandaa Mbadala Wake Kutoka Ujerumani

Josko Gvardiol anatajwa kuchukua mikoba ya Cesar Azpilicueta anayetarajiwa kutimkia nchini Hispania kwenye klabu ya Barcelona

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa beki na Nahodha wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Cesar Azpilicueta.

 

Barca imekuwa ikimnyemelea Azpilicueta kwa muda mrefu lakini Chelsea ilikuwa inatia ngumu kumuachia kabla ya kutafuta mbadala wake.

 

Azpilicueta ni moja kati ya wachezaji wachche ambao wamepata mafanikio makubwa katika klabu hiyo kwani amefanikiwa kutwaa mataji yote ya ngazi ya klabu akiwa na miamba hiyo ya soka ambao ni mabingwa wa dunia kwa ngazi ya vilabu.

Azpilicueta anatarajiwa kujiunga na Barcelona kutokea Chelsea

Kwa upande mwingine mlinzi wa RB Leipzig ya nchini Ujerumani Josko Gvardiol anatajwa kuelekea darajani kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Cesar Azpilicueta.

 

Leave a Comment