×

Rais Samia Amtaka IGP Mpya Kuonesha Ufanisi na Kuimarisha Usalama wa Raia

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kuapishwa kwa IGP  Wambura pamoja na Mabalozi mbalimbali

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema anatarajia kuona ufanisi mkubwa wa kazi kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Wambura ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa raia na mali zake.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 20, 2022 akiwa Ikulu Jijini Dodoma wakati anawapisha viongozi wateule akiwemo IGP mpya pamoja na Mabalozi mbalimbali walioteuliwa.

Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Aidha Rais Samia amesema Serikali inapanga kutazama kwa undani eneo la ajira, mafunzo, maadili na naidhamu kwa askari wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

 

“Lakini pia nmifumo ya ajira, mafunzo maadili na nidhamuhili pia ni eneo muhimu lazima tukalitizame kwa undani kwenye taasisi zote hizi zinazoshughulika na haki jinai kama nilivyotangulia kusema kwenye dunia ya leo haki za watu na haki za nchi lazima tuzipe kipaumbele.” Amesema Rais Samia.

 

Rais Samia amesisitiza kuhusu kuwepo kwa utaratibu maalum wa kupandisha vyeo kwa askari kwa kuzingatia kiwango cha elimu pamoja na mafunzo.

Leave a Comment