
MCHEZAJI raia wa Tanzania Simon Msuva (28) amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Al Qadsiah inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ya nchini Saudi Arabia.
Katika dili hilo Msuva anatarajiwa kukunya mkwanja wa kiasi cha dola 12000 kwa wiki ambayo ni sawa na shilingi milioni 28 za kitanzania ambayo kwa jumala kwa mwezi anavuta kiasi cha dola 50,000 ambayo ni sawa na shilingi milioni 117 za kitanzania.

Hivi karibuni Msuva amefanikiwa kushinda kesi yake ya madai dhidi ya klabu yake ya zamani ya Wydad Casablanca inayoshiriki Ligi Kuu ya soka nchini Morocco ambapo klabu hiyo iliamuriwa kumlipa mchezaji huyo kiasi cha shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.
Kulikuwa na taarifa nyingi zilizokuwa zikiendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikizihusisha klabu kubwa nchini za Simba na Yanga kutaka kuinasa saini ya mchezaji huyo lakini sasa ni rasmi Msuva atahudumu katika klabu hiyo yenye maskani yake nchini Saudi Arabia.