
PAMBANO ambalo lilisubiriwa na wapenzi wa ndondi kati ya bondia Anthony Joshua na Oleksandr Usyk linatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya Agosti 20 katika dimba la King Abdullah Sports City Saudi Arabia.
Katika pambano la kwanza lililofanyika katika uwanja wa Totenham hotspurs bondia alipoteza Anthony Joshua alipoteza pambano hilo lililofanyika semptemba 2021.
Anthony Joshua anaangalia uwezekano wa kurudisha mkanda wake alioupoteza katika pambano lake hilo la kwanza.

Oleksandr Usyk naye baada ya kutoka katika Jeshi la nchi yake ya Ukraine anatarajia kuutetea ubingwa wake huo.
Usyk alipata ruhusa ya kwenda kambi kwaajili ya kujiandaa kikamilifu ili kuweza kumkabili mpinzani wake katika pambano la marudiano.
Pambano hili linatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi ulimwenguni kutokana na namna pambano la kwanza lilivyoisha.