×

Mwananchi wa Kwanza Kupewa Mkopo wa Milioni 50 Kujenga Kituo cha Mafuta Kijijini

Waziri wa Nishati January Makamba akiongea na mwananchi anayefanya biashara ya kuuza mafuta kijijini Ugaka, Mkoani Tabora

WAZIRI wa Nishati, January Makamba bado yuko kwenye ziara yake ya Kijiji kwa Kijiji na amefanikiwa kufika Kijiji cha Ugaka wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

 

Akiwa kijijini Ugaka, Waziri wa Nishati kabla ya kuzungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara, alipata wasaa wa kuzungumza na Bw. Shaban Ali ambaye kwa sasa anafanya biashara ya mafuta kwa njia ya chupa na madumu kwenye Kijiji hicho.

Waziri Makamba akishuhudia utiaji wa mafuta kwenye bodaboda katika kijiji cha Ugaka mkoani Tabora

Mara baada ya kuzungumza nae Waziri Makamba amesema >> ‘Basi sisi tutakukopesha Milioni 50, Tumetenga Bilion 2 kama sehemu ya Majaribio kwa mwaka huu wa fedha sababu ni kwamba Wananchi Vijijini wanateseka kupata mafuta ambayo si salama lakini kwa bei ya juu’ – Waziri Makamba.

Vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kuhifadhia mafuta na mfanyabiashara huyo Mkoani Tabora

Mwananchi huyo anakua ni mnufaika wa kwanza atakayepata fedha za mkopo zilizotengwa na Serikali kupitia REA ili kuwawezesha wajasiriliamali kufungua vituo vidogo vya mafuta vijijini ili kuuza mafuta safi, kwa njia salama na kwa bei elekezi.

Leave a Comment