
DAR ES SALAAM, 26 Julai 2022. The African Development Bank’s Affirmative Finance Action for Women in Africa (AFAWA) Initiative imeandaa mpango wezeshi wa kwanza wa Fedha kwa ushirikiano na Mfuko wa Dhamana ya Afrika (AGF) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA). Mtiririko huo wa Fedha unaendelea juu ya ushirikiano uliopo kati ya AFAWA na AGF ambao unalenga kuziba pengo kwa ufadhili la Dola za Marekani bilioni 42 kwa wanawake wajasiriamali wadogo barani Afrika. (WSME )

Kuna mikakati ya biashara ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wanawake, sio tu kwa taasisi za fedha na wajasiriamali wanawake, lakini pia kwa ukuaji wa uchumi mkuu. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa AfDB, Ofisi ya Maendeleo ya Kanda ya Afrika Mashariki na Utoaji Biashara alisema, “Afrika Mashariki ni nyumbani kwa namna ya uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika. Mpango wa AFAWA unahakikisha wanawake wanaweza kupata fedha na mafunzo wanayohitaji ili kuchangia kikamilifu katika ukuaji huu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Mfuko wa Dhamana ya Afrika, Jules Ngankam alisema, “Afrika ni bara changa zaidi duniani, lakini wakati huohuo, nusu ya watu hao, idadi ya wanawake, bado iko mbali na kufikia uwezo wake katika kushiriki katika uundaji wa thamani.
Tunapoanza safari hii ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati wanawake nchini Tanzania, kupitia mpango wa AFAWA wa Dhamana ya Ukuaji, tuna matumaini makubwa kuwa matokeo hayo yatakuwa makubwa, na ya muda mrefu na yatachochea ukuaji wa uchumi.”
Kwa upande wake Esther Dassanou, Meneja wa AFAWA, alisema “AFAWA, kwa ushirikiano na Mfuko wa Dhamana ya Afrika, inafanyakazi moja kwa moja na taasisi za kifedha kote Afrika ili kuimarisha uwezo wao wa kuhudumia soko la wanawake, kuruhusu wanawake kuongeza biashara zao.
Mfululizo wa Mtiririko wa Fedha wa AFAWA nchini Tanzania ni wa kwanza kati ya hafla kadhaa zinazofanana tunazopanga kuandaa kote barani Afrika ili kuonyesha taasisi za kifedha faida za kibiashara na kiuchumi za kufadhili wajasiriamali wanawake.
AFAWA na AGF zinakaribisha taasisi za fedha nchini Tanzania kujiandikisha kwa ajili ya mpango wa Dhamana ya Ukuaji. “Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dk Akinwumi Adesina alipotembelea Tanzania Februari mwaka huu, alimuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa AFAWA itazinduliwa nchini,” Nnenna Nwabufo aliongeza. “Hii ni ahadi iliyotolewa na ahadi iliyotekelezwa. Nimefurahia sana kuwa sehemu ya hii.”
Nae Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ,Mh. Exaud Kigahe alisema “ Hii ni fursa kubwa kwa kuwawezesha wanawake wajasiriamali wadogo na wakati, uzinduzi huu utapelekea kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini. Sisi kama serikali tutahakikisha tunasimamia fursa hii ili iweze kufika kwa walengwa, na kauli mbiu yetu ni wezesha wanawake kiuchumi.
Rais wa Chama cha Mabenki Tanzania, Tuse Joune aliishukuru benki Maendeleo ya Afrika na Mfuko wa Dhamana ya Afrika kwa kuanzisha mpango huo ambao utahakikisha ukuaji wa wanawake wa dogo na wakati nchini Tanzania.
“Hii inaonyesha thamani ya kweli ya wanawake kwa uchumi wetu. Ni wakati muafaka kwamba tuhakikishe bidhaa za kibunifu ambazo zitakuwa sehemu ya ukuaji wa SME za wanawake, zikijibu mahitaji yao yote,” alisema.
Tukio hilo la siku tatu litajumuisha kikao cha mafunzo ili kuzipa taasisi za fedha ujuzi juu ya uwekezaji wa busara wa kijinsia na jinsi ya kutumia mpango wa Dhamana ya Ukuaji ili kuwa hatarisha wanawake wao wa SME.