×

Urusi Yasema Wafungwa 40 wa Ukraine Wameuawa Katika Mlipuko Uliofanywa na Vikosi vya Jeshi la Ukraine

Jengo lililopigwa na kombora linalodaiwa kuwa la wanajeshi wa Ukraine

WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imesema wafungwa 40 wa Ukraine wameuawa, kwa shambulio la makombora ya Ukraine katika Gereza moja kwenye Jimbo la Donetsk.

 

Maafisa wa Urusi wamedai kuwa wafungwa wengine 75, wamejeruhiwa katika Shambulio la Roketi kwenye kambi ya Magereza huko Olenivka.

Mapigano makali yanaendelea katika Jimbo la Donetsk baina ya vikosi vya Ukraine na Urusi

Aidha Jeshi la Ukraine limekanusha madai hayo na badala yake limeishutumu Urusi kwa kushambulia Jela hiyo, limesema Moscow imefanya hivyo kutafuta kuficha ushaidi wa mateso katika eneo hilo.

 

Mkuu wa wafanyakazi wa Ukraine alisema:

 

“Adui wa Ukraine anaendelea na mbinu zake za Propaganda za kuendesha Vita vya hila hili kushutumu Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine kwa kushamulia Miundombinu ya Raia na Idadi ya Watu, akificha vitendo vyake vya hila”

 

Kanda za Runinga za Serikali ya Urusi zinaonyesha mabaki ya moshi na jengo ambalo linaonekana kuwa na baadhi ya Mabaki ya Binadamu, ambapo uchanganuzi unaonesha kuwa Jengo hilo lilipigwa na kifaa cha kuwasha Moto na sio silaha za kawaida.

 

Daniil Bezsonov, Msemaji wa Jamuhuri ya Watu wa Donetsk inayoungwa mkono na na Urusi amesema kuwa idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka.

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imekanusha kuhusika katika shambulio hilo

Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema kuwa shambulio hilo limefanywa kwa silaha za Kivita zinazoitwa ‘Himars’ zilizotengenezwa Marekani na kuishutumu Ukraine kwa uchochezi uliofanya kwa makusudi.

 

Msemaji wa Wizara hiyo, Lt Jenerali Igor Konashenkov, amesema Wafanyakazi wa Magereza wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

 

Lakini Mykhailo Podolyak, ambaye ni Mshauri wa Rais wa Ukraine Vladmir Zelensky amesema madai hayo ya Urusi ni Operesheni ya Uongo wa hali ya juu na ya Kijinga iliyoundwa ili kudharau Mamlaka ya Ukraine.

Leave a Comment