×

Mtu Mmoja Akutwa Amefariki Mto Thames Uingereza, Tahadhari Yatolewa

Askari Polisi wakiwa kazini

KIJANA wa kiume anayesadikiwa kuwa na umri wa miaka 20 amekutwa amefariki katika mto Thames jiji la London nchini Uingereza.

 

Polisi kitengo cha dharura walipokea simu kuhusu mtu aliyeonekana ndani ya maji mida ya saa kumi jioni siku ya Jumapili.

 

Mwili wa mwanamume huyo, anayeaminika kuwa na umri wa miaka 20, ulitolewa kutoka mtoni mida ya saa nne usiku wa Jumapili na wapiga mbizi wa Polisi.

 

Ndugu zake wa karibu wamearifiwa na Polisi kuhusu kifo cha kijana huyo.

Watu wametahadharishwa kuwa makini kucheza maeneo ya mtoni hasa nyakati za usiku

Kaimu Kamanda wa Polisi Kusini Magharibi, Richard Smith, alisema: “Mawazo na maombi yetu yameenda kwa kijana ambae amepoteza Maisha yake”

“Maafisa wetu walifanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na wananchi lakini licha ya jitihada hizo hatukuweza kuokoa Maisha yake”

“Lazima nirudie tena kwa huzuni hatari ambayo maji huleta, Inaweza kuonekana si ya kutisha lakini hatari ya maji ni kubwa na hata kupoteza maisha, tafadhali usiingie majini wakati wowote bila kufuata njia salama. Madhara yake ni makubwa na hatutaki kuona familia nyingine zikipata habari mbaya kama hii.”

 

Kufuatia kipindi kirefu cha hali ya hewa ya joto, Uingereza sasa inakabiliana na mvua za radi kwa siku kadhaa ,lakini mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakaleta hatari zaidi badala ya ahueni, wataalamu wa hali ya hewa wameonya.

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment