
BAADA ya kupoteza mechi dhidi ya Brentford kwa mabao manne kwa sifuri watu wengi walitaka kusikia nini kitatokea juu ya mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo.
Mfululizo wa matokeo mabaya umezidi kumuweka Ronaldo katika hali ngumu ikizingatiwa kuwa alihusishwa na kuomba kuachana na klabu hiyo
Mshambuliaji huyo wa Kireno ambaye amepata mafanikio mengi katika mpira wa miguu anataka kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Mchezaji huyo namba mbili kwa tuzo za mchezaji bora duniani ameshinda Ballon D’or mara tano nyuma ya Lionel Messi mwenye tuzo hizo saba.
Msemaji wa klabu ya Manchester united ya Uingereza ameendelea kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi na hakuna mabadiliko ya nafasi kwa mshambuliaji huyo ataendelea kuwa chaguo katika nafasi ya ushambuliaji.
Klabu ya Manchester United imeshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi mbili za kwanza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992.