×

Wawili Wafariki na Kadhaa Kujeruhiwa Katika Mlipuko wa Soko Nchini Armenia

Mlipuko mkubwa umetokea kwenye soko nchini Armenia

MLIPUKO huo ulitokea katika eneo la kuhifadhi baruti ndani ya soko la Surmalu katika mji mkuu wa Armenia, Yerevan, Jumapili alasiri na kusababisha mlipuko.

 

Moto mkubwa ulizuka huku ukiambatana na moshi mzito uliotanda juu ya anga na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine kujeruhiwa.

Juhudi za uokoaji zinaendela 

Taarifa ya Wizara ilisema kulikuwa na ripoti zaidi ya 20 kutoka kwa watu ambao walisema hawakuwaona ndugu zao ambao walikuwa ndani ya soko.

 

Jumuiya ya Wanahabari ilisema mmoja wa waandishi wake aliona watu wawili wakitoka kwenye kifusi – mwanamke aliye na jeraha la mguu na kijana ambaye alionekana kuwa na hali mbaya.

 

Wafanyikazi wa uokoaji walilazimika kufanya kazi usiku kucha wakiamini bado kuna watu watakuwa mamenasa chini ya vifusi na vyuma vilivyotokana na majengo yaliyo bomoka.

 

Hakukuwa na taarifa yoyote rasmi ya kisababishi cha moto katika soko, huku Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi juu ya moto huo.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment