×

Uingereza Imekuwa Nchi ya Kwanza Kuidhinisha Chanjo ya Aina Mbili za Corona

Chanjo mpya iliyoidhinishwa na Serikali ya Uingereza

UINGEREZA ndiyo nchi ya kwanza kuidhinisha matumizi ya chanjo iliyoundwa kulenga aina mbili tofauti za virusi vya Corona ambavyo ni kirusi cha zamani (Uviko-19) na kirusi kipya cha Omicron inayojulikana kama “Spikevax bivalent Original/Omicron” ambayo imetajwa kuwa bora kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18.

 

Serikali imesema chanjo hiyo sasa itakuwa sehemu kubwa ya kampeni ya kupambana dhidi ya Corona.

Virusi vya Corona vilianza kwa mara ya kwanza Wuhan nchini China mnamo mwaka 2019

Maafisa wa Afya wanashauri watu kupata chanjo hiyo mpya hata kama ulishapata ile ya zamani kwa kuwa chanjo za awali zilizotumiwa katika janga hili ziliundwa kusaidia mwili kupigana na aina ya kwanza ya virusi ambayo iliibuka huko Wuhan, China, mwishoni mwa 2019, lakini virusi vya Corona tangu wakati huo vimebadilika sana, na vinaweza kukwepa baadhi ya ulinzi wetu wa kinga na kuleta madhara.

 

Chanjo ya zamani bado inauwezo wa kutoa kinga kali dhidi ya kuwa mgonjwa sana au kufa, lakini kampuni zinazibadilisha ili zilingane na jinsi virusi vinavyobadilika, huku kesi za Corona kwa sasa zikipungua kwa kasi nchini Uingereza.

 

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment