
RAIS wa Korea Kusini Yoon Suk-Yeol atoa wito wa kuwepo kwa diplomasia yenye lengo la kujenga amani endelevu kati ya wapinzani hao huku kukiwa na mvutano kuhusu mpango wa kuendeleza silaha wa Korea Kaskazini.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatano, Bw Yoon alisema hataki mabadiliko ya kisiasa nchini Korea Kaskazini ambayo yameletwa kwa nguvu na akahimiza Kaskazini kurejea kwenye mazungumzo yanayolenga kubadilishana hatua za kuondoa silaha za nyuklia kwa manufaa ya kiuchumi.

Wito wa mazungumzo unakuja licha ya vitisho vilivyotolewa na dadake Kim Jong Un huku akilaumiwa kwa vipeperushi vya propaganda kutoka Korea Kusini vilivyopatikana karibu na mpaka kwa kusababisha milipuko ya Covid-19.

Makombora hayo yalirushwa kutoka mji wa pwani ya magharibi wa Onchon mapema Jumatano, chanzo cha jeshi la Korea Kusini kilisema.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao