MBUNGE wa Viti Maalum mkoa wa Mara (CCM) Juliana Masaburi amefanya mkutano na watu wenye ulemavu wa ngozi wilaya ya Musoma vijijini na kuwapa mafuta yanayosaidia kuwakinga na mionzi ya jua.

Mbunge Juliana ametoa mafuta yenye thamani ya milioni 1.8 kwa walemavu hao na kuwaeleza kuwa na ulemavu hakuzuii wao kuwa tegemezi kwa Taifa na wamuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea Maendeleo.
Pia Mhe. Juliana amehamasisha Swala zima la sensa ya watu na makazi kwani ni jukumu la kila mtanzania kujitokeza kuhesabiwa kwa maendeleo ya Taifa