×

Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden Akutwa na Covid-19, Mmewe Yupo Salama

Jill Biden Mke wa Rais wa Marekani

IKULU ya marekani (White House) imethibitisha kuwa mke wa Rais huyo wa Marekani Jill Biden Alipatikana na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.

 

Jill Biden mwenye miaka 71 alipimwa na hakukutwa na maambukizi siku ya Jumatatu wakati wa kikao cha kawaida cha upimaji, lakini alipata dalili kama za Covid-19 jioni hiyo.

 

 

Alipimwa hasi kwenye kipimo cha haraka cha antijeni kabla ya kipimo cha PCR kutumika na kuonyesha majibu chanya.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mke wake Jill Biden

Msemaji Elizabeth Alexander alisema kuwa, kama ilivyokuwa kwa mume wake Joe Biden, Jill Biden amepata chanjo mbili na jabs mbili za kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa huo.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment