
MKUU wa jeshi la Polisi nchini Somalia amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo ambalo limefanywa na wanamgambo wa al shabaab ambapo kundi hilo lina uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la al Qaida.
Katika shambulio hilo Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Jenerali Abdi Hassan Hijar alisema kwamba miongoni mwa watu waliokufa ni raia wa kawaida, pamoja na maafisa wa usalama, baada ya shambulizi hilo kwenye hoteli ya Hayat, iliyoko kati kati ya mji wa Mogadishu, karibu na makao makuu ya idara ya uchunguzi wa kihalifu.

Mkuu huyo wa jeshi amesema jukumu kubwa la maafisa wake lilikuwa kuwaokoa watu waliokwama ndani baada ya wapiganaji wa al Shabab kuishambulia hoteli hiyo kwa mabomu ya mlipuko, na kulivamia jengo hilo ambapo mapambano ya risasi yalifuatia na kudumu kwa takribani saa 30.
Katika Oparesheni hiyo watu Zaidi ya 106 waliokolewa wakiwemo wanawake na watoto, watu hao walifanikiwa kuokolewa na maafisa wa Polisi baada ya mapigano yaliyokuwa yakiendelea.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao