×

Kampuni ya Kuuza Mafuta ya TotalEnergies Nchini Ufaransa Yashutumiwa Kusambaza Mafuta ya Ndege Kwa Jeshi la Urusi

Waziri wa Uchukuzi Ufaransa

WAZIRI wa Uchukuzi wa Ufaransa Clement Bon alitoa wito wa kuchunguza kashfa hiyo ya tuhuma za kampuni ya mafuta ya TotalEnergies kusambazia Urusi mafuta kwa mahitaji ya jeshi la anga la Urusi.

 

TotalEnergies bado inamiliki karibu nusu ya hisa katika uwanja wa gesi nchini Urusi.

Kampuni ya kuuza mafuta ya TotalEnergies

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinadai kuwa gesi inayozalishwa na kampuni ya TotalEnergies inatumika kuzalisha mafuta ya ndege ambayo yanasambazwa kwa Jeshi la anga nchini Urusi.

 

Usimamizi wa kampuni ya TotalEnergies nchini Ufaransa ulitupilia mbali madai haya na kusema kuwa hayana msingi.

 

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi wa Ufaransa Clement Bon aliingilia kati nakusema kuwa “Hii ni mada nzito sana” kwenye kituo cha TV cha France 2. “Kwa hivyo, ni muhimu kujua kama kumekuwepo – sio muhimu sana iwe ni kwa makusudi au la – ukiukaji wa sheria ya vikwazo au matumizi mabaya ya nishati inayozalishwa na kampuni yoyote – ya Ufaransa au nyingine yoyote’’.

 

Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment