
MCHEZAJI wa klabu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang amevamiwa na watu wenye silaha nyumbani kwake jijini Barcelona, imeripotiwa kwamba wavamizi wamefanikiwa kuchukua baadhi ya vitu vya thamani na kumshushia kipigo mchezaji huyo.

Watu wanne wenye silaha walivamia makazi ya mchezaji huyo ambaye anahusishwa na tetesi za kurejea katika ligi kuu ya uingereza, polisi wanasema hawakuishia kuchukua mali tu walimpiga pia Aubameyang katika tukio hilo pamoja na kumtishia kisu mke wa mchezaji huyo wakati wakitafuta upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.

Matukio kadhaa ya uvamizi kwa wachezaji wakubwa yaliwahi kuripotiwa katika jiji hilo japokuwa mara nyingi uvamizi hufanyika wakati wachezaji wakiwa hawapo majumbani mwao jambo lililofanya uvamizi huu kuwa wa tofauti kidogo.
Polisi wamesema wanaendelea na msako kuwabaini walliohusika na tukio hilo huku Aubameyang akipanga kuondoka mapema Zaidi ya alivyopanga kutoka katika makazi hayo.
Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.