
Waziri wa hali ya hewa nchini Pakstani Sherry Rehman amesema kuwa mafuriko yanayondelea nchini humo yameleta hasara kubwa ambapo karibu theluthi moja ya ardhi imesombwa na maji.
Pia waziri huyo alisema kuwa mafuriko hayo yamesomba barabara, nyumba na mimea na kuacha uharibifu mkubwa katika maeneo tofautitofauti nchini humo, “Kote ni kama bahari kubwa hukuna ardhi kavu ya kusukuma maji nje” alisema waziri.

Maafisa nchini humo walisema jana kuwa karibia watu 1,136 wamefariki dunia kutokana na mafuriko hayo yaliyoanza tangu msimu wa masika mwezi Juni, mwaka huu.

Pia waziri wa mambo ya nje nchini humo Bilawal Bhuto zardar alisema kuwa theluthi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko hayo wanaamika kuwa ni Watoto, “Bado tunaendelea kutathimini ukubwa wa uharibifu “ alisema waziri huyo.
Imeandikwa na Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.