
UKRAINE imedai kuwa imeshambulia na kuaribu kabisa madaraja, maghala ya silaha pamoja na vituo vya kuongoza shughuli za kijeshi katika eneo linalodhibitiwana majeshi ya Urusi kusini mwa Ukraine.
Urusi nayo imesema kuwa imelipiza shambulizi hilo kwa kuwauwa wanajeshi kadhaa wa jeshi la Ukraine, mapigano hayo yametokea katika eneo la Kherson ambako wanajeshi wa Urusi walipata mafanikio makubwa ya kulidhibiti eneo hilo mwanzoni mwa vita nchini Ukraine.

Mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wa Ukraine yamezidisha tetesi kuhusu Operesheni yake iliyokuwa imeandaliwa kwa muda mlefu dhidi ya Urusi.
Wizara ya ulinzi ya Uingereza kupitia ripoti yake ya kiintelijensia imesema wanajeshi wengi wa Ukraine wameimarisha mashambulizi ya makombora katika eneo la kusini lianalodhibitiwa na Urusi.
Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao