×

Watu 18 Wauawa kwa Kupigwa Risasi, 34 Wajeruhiwa na 9 Mahututi Madagascar

Polisi walifyatua risasi kwa waandamanaji nchini Madagascar

WATU 18 wameuawa na wengine 34 kujeruhiwa huku 9 wakiwa mahututi, baada ya Polisi kufyatua risasi kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, ripoti hiyo imetolewa na Tango Oscar Toky ambaye ni daktari mkuu kwenye hospitali moja iliyopo Kusini Mashariki mwa Madagascar.

 

Toky ameongeza kwamba wanasubiri helikopta za serikali ili kuwapeleka majeruhi kwenye hospitali ya mji mkuu wa nchi hiyo.

 

Maelfu ya watu waliandamana baada ya kukasirishwa kutokana na kutekwa nyara kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi au albino.

 

Takriban watu 500 walikuwa wamebeba visu na mapanga walijaribu kuingia kwa nguvu kwenye kituo cha polisi ambacho washukiwa wa utekaji nyara walikuwa wameshikiliwa.

Waandamanaji Madagascar

Afisa wa polisi kutoka Mji wa Ikongo uliopo takribani kilometa 90 Kusini Mashariki mwa Mji Mkuu wa Antananarivo, amesema kwamba walijaribu kuzungumza na waandamanaji, lakini walikataa na hawakuwa na njia nyengine zaidi ya kutumia risasi za moto kwa ajili ya kujilinda.

 

Mkuu wa Polisi kitaifa, Andry Rakotondrazaka amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba tukio hilo ni la kuhuzunisha na kubainisha kuwa lingeweza kuzuilika.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment