×

Hospitali Yashambuliwa kwa Makombora na Majengo Kuharibika Vibaya Ethiopia

Mlipuko uliotokea nchini Ethiopia

VURUGU zimeongezeka nchini Ethiopia na kushambulia majengo mbalimbali likiwemo jengo moja la hospital iliyopo kwenye eneo la Mekele katika Jimbo la Tigray nchini humo.

 

Mkurugenzi wa hospitali ya Ayder mnamo Agosti 31, 2022 alitoa tahadhari kuhusu vurugu hizo na baada ya muda mfupi likatokea shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya eneo la Mekele.

 

Kulingana na msemaji wa waasi wa TPLF, mabomu matatu yalirushwa katika hospitali ya Mekele huku vyanzo vingine vya ndani vinahakikisha kwamba baadhi ya majengo ya hospitali hii yameharibika kutokana na shambulio hilo.

 

TPLF limehakikisha kwa namna yoyote ile ngome au kambi za kijeshi hazitalengwa na mashambulizi haya mapya yaliyoanza katika eneo hilo.

Uharibifu wa miundombinu

Hayo yamejiri baada ya wiki iliyopita kutokea shambulio la bomu katika shule ya chekechea huko Mekele ambapo Jeshi la Ethiopia lilihakikisha kwamba linashambulia kambi za kijeshi tu.

 

Serikali ya Ethiopia inawatuhumu waasi wa Tigray kwa kuanzisha tena mashambulizi kuelekea mpaka kati ya nchi hiyo na Sudan ambapo mapigano hayo yanadaiwa kuendelea.

Majengo yameharibiwa vibaya

Mapema wiki hii TPLF ilifanya mashambulizi yake huko Amhara nje ya mipaka ya Tigray kisha kuelekea mji muhimu wa Weldiya pamoja na eneo la Afar.

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment