Rais Samia Afika Kuhani Msiba wa Mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi
Global Publishers September 1, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpa pole Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Mwinyi mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Chukwani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuhani msiba tarehe 01 Septemba, 2022
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 1, 2022 amefika nyumbani kwa marehemu, Chukwani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuhani msiba ambapo amepokelewa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Mwinyi.
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais wa Zanzibar mara baada ya kuhani msiba nyumbani kwa Marehemu Chukwani mjini Zanzibar tarehe 01 Septemba, 2022Rais Samiaakiagana na Mama Siti Mwinyi baada ya kuhani msiba wa mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi nyumbani kwa Marehemu Chukwani mjini Zanzibar tarehe 01 Septemba, 2022