×

Uingereza Yaelekea Kupata Waziri Mkuu Mpya Wiki Ijayo 

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Liz Truss

UINGEREZA inaelekea kuwa na Waziri Mkuu mpya baada ya Waziri Mkuu wao wa zamani Boris Johnson kujiuzulu mwezi Julai kufuatia mfululiza wa kashfa dhidi yake.

 

Wanachama wa chama cha Conservatives watamchagua mrithi wa Waziri Mkuu wa zamani  Boris Johnson.

 

Machaguo ya wanachama wa Conservatives ni  chancellor wa zamani Rishi Sunak au waziri wa sasa wa mambo ya nje Liz Truss.

 

Lakini kwa sasa Liz Truss ndiye anaye ongoza kwa kura za maoni kwa sasa.

 

Mbali na hayo Waziri Mkuu mpya wa Uingereza atakumbwa na changamoto za vita vinavyoendelea nchini Ukraine kwakua Uingereza tayari imetoa msaada wa Dola bilioni 2.7 kwaajili ya msaada wa silaha za kivita nchini Ukraine tangu Urusi ilipo vamia nchi hiyo mwezi Februari.

Waziri Mkuu wa Uingereza aliyetoka Madarakani Boris Johnson

Uingereza imechukua nafasi ya pili chini ya Marekani kwaku toa msaada wa pesa nyingi kuisapoti nchi ya Ukraine kwenye mapambano yake dhidi ya Urusi.

 

Mchambuzi wa mambo ya siasa wa chuo cha King’s College mjini London Alan Wagner amesema kwamba “Johnson alikuwa rafiki wa karibu wa Kyiv, na kwamba huenda mambo yakawa tofauti chini ya utawala wa Truss “. Alan anasema kwamba huenda Lizz Truss anaye ongoza kwa kura za maoni akawekeza zaidi kwenye ulinzi wa taifa pamoja na kukuza uchumi.

 

Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.

 

 

Leave a Comment