
DAKTARI wa kujitolea raia wa nchini uingereza Craig Mackintosh amepoteza maisha nchini Ukraine, Dada wa marehemu aitwae Lorna alisema kaka yake alipoteza maisha akiwa kazini baada ya kusafiri kwenda Ukraine kusaidia wahanga kufuatia uvamizi wa Urusi huko nchini Ukraine.
Lorna alisema kaka yake amepoteza maisha akiwa kazini kuunga jitihada za Ukraine kupambana na vikosi vya Urusi.
Katika maombi ya msaada wakifedha ( GoFundMe ) iliyoundwa kuleta mwili wake nyumbani alifichua kuwa aliuawa nchini Ukraine mnamo tarehe 24 Agosti “Tafadhali tusaidie kumrudisha shujaa huyu wa vita nyumbani, ndugu yetu alijitolea kwa ujasiri kwenda Ukraine kama daktari kusaidia kuokoa maisha katika nchi hii iliyokumbwa na vita ” aliandika Lorna

“Akiwa katika jukumu la kusaidia wengine alipoteza maisha. Mtu huyu asiyejitolea kwa sasa amekwama katika chumba cha kuhifadhia maiti nchini Ukraine na hakuna msaada wa kumrudisha nyumbani.”
Alisema ingegharimu karibu £4,000 kurejesha mwili wake nchini Uingereza, “Tumezungumza na mtoa huduma wa mazishi wa kimataifa na itagharimu takriban £4,000 kumrejesha nchini Uingereza, alitoa maisha yake kuokoa wengine na anahitaji kurejea nyumbani ili kupata mazishi anayostahili. Mazishi ya shujaa wa kweli akizungukwa na familia yake na marafiki. Tafadhali, tafadhali saidia kumleta shujaa wetu nyumbani.”
Kufikia Jumatano jioni, GoFundMe ilikuwa imevuka lengo lake, na kuongeza £4,590.
Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.