×

RC Mgumba Aupongeza Mfuko wa Self Microfinance Kwa Kukuza Mtaji Wake

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameupongeza Mfuko wa Self Microfinance kwa kuweza kukuza mitaji yao kutoka Bilioni 57 mwaka June 2016 hadi kufikia Bilioni 59.8 June 2022 jambo ambalo ni muhimu kwa ustawi wake.

 

Mgumba aliyasema hayo leo wakati akifungua matawi manne ya Mfuko huo ambapo alisema kwani zipo taasisi nyingi zimepewa mbegu mifuko mengine na Serikali lakini imekufa maana yake walikula lakini nyie ni taasisi inafaa zaidi na kuungwa mkono kwa kuweka mbegu zaidi kwa sababu mtaji upo salama na inaendelea kukua siku hadi siku.

Mkuu huyo alisema amefarijika zaidi kwa mpango mkakati wa kuhakikisha wanaongeza matawi ili kufika mikoa yote ikiwemo kufarijika kuona Mfuko huo unatekezwa n kufanya kazi nchi mzima Tanzania bara ba Visiwani.

Alisema kwamba Serikali inafahamu Mfuko wa Self ni moja ya taasisi muhimu ya fedha katika maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi na kichocheo cha uchumi na ustawi wa maendeleo

Leave a Comment