×

Nyuklia Yatumika Kupata Umeme Katika Umoja wa Falme za Kiarabu

Nyuklia

KUTOKA nchni Emirate Kampuni inayoitwa Emirates Nuclear Energy Corporation (ENEC) wao wamekuja na njia ya tofauti ya kupata umeme, ambapo wao hutumia nguvu ya nyuklia kupata umeme na siyo kwa ajili ya vifaa vya kivita.

 

Kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2009 chini ya Rais wa nchi za umoja wa falme za kiarabu yaani” United Arab Emirates” (UAE) Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Kiongozi huyu ndiye aliye elekeza kuanzishwa kwa matumizi ya nguvu za Nyuklia ili kupambana na mahitaji ya umeme katika nchi zenye mahitaji ya umeme wa uhakika.

Mionzi ya Nyuklia

Kipande kidogo cha nyuklia ni sawa na lita 500 za mafuta lakini pia kama haitoshi kipande hichohicho kidogo cha nyuklia ni sawa na tani moja za makaa ya mawe pia kinaweza kuwasha umeme kwenye nyumba kwa miezi minne(4) bila
kukatika wala shida yoyote.

Leave a Comment