
KIONGOZI wa Chama cha mlengo nchini Italia Matteo Salvini, amezua gumzo nchini humo baada ya kusema kuwa vikwazo ilivyowekewa Urusi na mataifa ya Magharibi kufuatia Taifa hilo kuivamia Ukraine havifanyi kazi.
Salvini amesema miezi kadhaa imepita na watu wanaendelea kulipa gharama ya mara mbili hadi nne ya bei ya nishati kuliko walivyokuwa wakilipa hapo mwanzo huku akisema vita bado vipo na Urusi inaendelea kunufaika.

Kupanda maradufu kwa bei ya nishati ya gesi tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine kumeyumbisha uchumi wa mataifa kadhaa ya Ulaya ambayo kabla ya vita yalikuwa tegemezi wa gesi kutoka Urusi.
Imeandikwana: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.