×

Fahamu Kuhusu Mapambano ya Ndondi Yaliyoisha kwa Kustaajabisha

UKIACHANA na Pambano lililowakutanisha Hassan Mwakinyo na Muingereza Liam Smith lililomalizika kwa mwakinyo kusalimu amri bila watu kujua kilichotokea.

 

Mapambano mengine ambayo yaliisha kwa kuwaacha watu katika sintofahamu ni haya.

 

Lennox Lewis vs Oliver McCall II

Katika pambano hili lililofanyika 1997 liliwakutanisha mabondia hao na lilikua pambano la kugombania mkanda wa WBC. Pambano hilo lililofanyika Marekani katika mji wa Las Vegas.

Lennox Lewis vs Oliver McCall

Pambano hili lilikua la kustaajabisha baada ya bondia Oliver McCall katika rmzunguko wan ne kukataa kurusha ngumi na kuonekana kama amesusia mchezo huo.

 

Lewis aliendelea kumrushia makonde tu, muamuzi aliamua kumaliza pambano, kwa sababu  halikuwa pambano la ngumi, bali pambano na mrusha ngumi na mkinga ngumi.

 

Evander Holyfield vs Mike Tyson

Pamabano hili lililokuw la kustaajabisha baada ya bondia Mike Tyson Kumg’ata mpinzani wake Evander. Pambano hili lilichukua umaarufu baada ya tukio hili kufanywa na mwana masumbwi bora zaidi.

Evander Holyfied na Mike Tyson

Pambano hili lililopewa jina la the bite fight kutokana na Tyson kumg’ata Evander Mara mbili kwenye raundi ya tatu. Mwamuzi aliamua kumaliza pambano hilo lililofanyika tarehe 28 mwezi Juni 1997.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment