×

Nini Kinafuata Baada ya Rais Mteule William Ruto Kuidhinishwa na Mahakama?

Rais Mteule William Ruto.

Rais Mteule William Ruto anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne, Septemba 13, 2022.

Hii ni baada ya Mahakama ya Juu Zaidi kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa urais katika uchaguzi uliofanyika Agosti 9 na mpinzani wake mkuu ambaye pia ni kiongozi wa Muungano wa Azimio, Raila Odinga.

 

Kawaida, kutakuwa na shughuli nyingi zitakazo shuhudiwa wiki moja kabla ya sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Rais mteule William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua.

 

Kikatiba, sherehe hiyo inafanyika siku ya saba tangu tarehe ambayo Mahakama ya Juu Zaidi imetoa uamuzi wake kutokana na kesi yoyote ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyowasilishwa.

 

Rais Mteule hushika madaraka kwa kula kiapo au uthibitisho wa uaminifu, wa utekelezaji majukumu ya ofisi.

Sherehe za kukabidhi mamlaka huandaliwa na kamati maalum ya kula kiapo cha rais inayoongozwa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Joseph Kinyua.

 

Rais mteule atatwaa hatamu za uongozi kwa kula kiapo cha kukubali majukumu yaliyotwikwa katika ofisi ya urais kwa mujibu wa sheria.

Wakati wa sherehe hiyo, Rais mteule anapaswa kuapishwa hadharani na Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu iwapo Jaji Mkuu hatakuwepo.

 

Baada ya kula kiapo, Rais atatia saini cheti cha kuapishwa kwake huku rais anayeondoka akimkabidhi vifaa vya mamlaka na uongozi: upanga na katiba.

 

Rais atashika madaraka yake kwa muhula unaoanzia tarehe ambayo aliapishwa, na kuishia wakati mtu anayefuata aliyechaguliwa kuwa rais anapoapishwa.

BABU wa YANGA AMLILIA MANARA, NI YULE ANAYE – TRENDI MITANDAONI – ”NI MTU MUHIMU, WANATUONEA”..

Leave a Comment