×

Rais Kenyatta Akosoa Uamuzi wa Mahakama wa Kutupilia Mbali Ombi la Raila Odinga

Uhuru Kenyatta akiwa na Rais mteule William Samoei Ruto

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye anamaliza muda wake kama Rais wa nchi hiyo amesema atahakikisha wanakabidhiana madaraka kwa amani na Rais mteule William Samoei Ruto.

 

Katika ujumbe uliorekodiwa na kuwekwa kwenye mtandao wa You Tube, Kenyatta hata hivyo ameonekana kukosoa uamuzi wa Mahakama ya juu uliotupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa William Ruto.

Rais Kenyatta anayemaliza muda wake wa Urais

“Hatua ya kukabidhi madaraka imeanza, ikisimamiwa na kamati iliyoundwa kufanikisha shughuli hiyo, na iliyoanza kazi Agosti tarehe 10. Nia yangu ni kuhakikisha kwamba shughuli ya kupokezana madaraka inafanyika kwa njia nzuri kabisa,” amesema Uhuru.

Rais mteule William Ruto, Rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta na Raila Odinga

“Ni jukumu la kila mkenya kudadisi kwa undani kabisa na kutafuta ukweli kuhusu maamuzi yanayofanywa na taasisi za kikatiba na kuzifanyia majaribio ili kuhakikisha kwamba maamuzi yanayotolewa ni sawa” aliendelea kuongea Uhuru Kenyata.

Uhuru Kenyatta amemuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka huu 2022 licha ya ahadi aliyokuwa ametoa kwamba angemuunga mkono Naibu wake Dr. William Ruto wakati anapomaliza muda wake wa mihula miwili madarakani.

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Mitandao

 

Leave a Comment