×

Takribani Maelfu ya Watu Wamehamishwa Korea Kusini kwa Kuvamiwa na Kimbunga

Mafuriko yaliyo sababishwa na vua kali ikiambatana na kimbunga

KIMBUNGA chenye nguvu Zaidi ambacho hakikuwahi kuikumba Korea Kusini kwa miaka mingi kimekumba eneo lake la kusini, kiki ambatana na mvua ilionyesha karibu mita moja ambayo ni sawa saw ana futi 3 na kuharibu barabara, kuangusha nyaya za umeme baada ya maelfu ya watu kuhamishwa na kupelekwa kwenye ardhi ambayo haijakumbwa na tatizo hilo.

 

Kimbunga Hinnamnor kilipitia kisiwa cha mapumziko cha Jeju na kuanguka kusini mwa nchi karibu na bandari ya Busan mapema Jumanne, mamlaka ilisema, huku mvua kubwa na upepo mkali vikitarajiwa kuendelea kutwa nzima.

Mafuriko Korea kusini

Waziri Mkuu Han Duk-soo alitoa wito wa kuhamishwa katika maeneo ambayo yanaweza kukumbwa na mafuriko, akisema Hinnamnor inaweza kuishia kuwa “kimbunga kikali kihistoria ambacho hatukuwahi kukumbana nacho hapo awali”.

 

Takribani nyumba 20,000 ziliachwa bila umeme katika wilaya za kusini kutokana na upepo kuangusha nyaya za umeme.

 

Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment