×

Uwezo wa Nyuklia Kwenye Serikali ya Kigeni Yahusishwa Kwenye Hati ya Trump

Donald Trump

GAZETI la Washington Post liliripoti kwamba miongoni mwa nyaraka zilizopatikana na maajenti wa FBI katika kituo cha mapumziko cha Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump mwezi uliopita ni moja inayoelezea ulinzi wa kijeshi wa nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa nyuklia.

 

Pia kuna baadhi ya nyaraka zilipatikana kaitika msako huo zilikuwa zikielezea operesheni za Marekani ambazo ni za siri kiasi kwamba maafisa wengi wakuu wa usalama wa taifa hawajui kuzihusu, Agost 8 katika eneo ambalo hupumzika rais huyo mstaafu Donald Trump la Mar-a-Lago.

Maajenti wa FBI

Takribani ya nyara kamilioni na laki moja zilikamatwa katika msako wa Agosti8 na kati ya nyaraka miamoja zilikuwa zimewekwa alama kubainisha kwamba ziliainishwa.

 

Trump aliondoka madarakani Januari 2021 na kurudisha hati mnamo Januari na juni mwaka huu. Lakini nyaraka zilizorudishwa ni chache kuliko ambazo zimekutwa katika mapumziko ya rais huyo mstaafu.

 

Imeandikwa: leocardia Charles kwamsaada wa mitandao.

Leave a Comment