×

Klopp Akiri Liverpool Lazima Wajipange Upya Baada ya Kipigo Dhidi ya Napoli

Klopp akiri Liverpool lazima wajipange upya

KOCHA mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kwamba timu yake ya Liverpool inahitaji kujipanga upya baada ya kipigo cha goli 4 kwa 1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

 

Liverpool waliruhusu mabao matatu katika kipindi cha kwanza kabla ya kufungwa bao la nne katika hatua za mwanzo za kipindi cha pili. Luis Diaz aliifungia Liverpool bao la kufutia machozi, lakini timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza haikuonekana kurejea mchezoni

 

Kikosi cha Klopp sasa kimeshinda mechi mbili pekee kati ya saba za kwanza za msimu huu, na kocha huyo wa Ujerumani anaamini mabadiliko makubwa yanahitajika ili kubadilisha mambo.

Wameshinda mechi mbili tu kati ya saba msimu huu

“Tulicheza vibaya katika kipindi cha kwanza lakini kwa kawaida huwa haturuhusu mabao matatu,

“Tuna Wolves Jumamosi na kama wameangalia mchezo usiku wa leo, hawawezi kuacha kucheka, watasema na sisi pia ni wakati mwafaka wa kuwacheza nao, lazima tujipange vizuri zaidi katika kila kitu,” alisema Klopp.

 

Klopp ameitaka timu yake kukaa chini na kutafuta suluhu ili kurejea katika ubora wao.

Kloop ameitaka timu kukaa chini kutafuta suluhu

“Hatuchezi vizuri vya kutosha, hiyo ni dhahiri na ndiyo maana tunapoteza michezo, kuna kazi ya kufanya, ni jukumu langu na ninahitaji muda wa kufikiria. Kuna mambo machache dhahiri na inabidi tuyaweke.” Alisema klopp

 

Imeandikwa na:John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment