
ILITANGAZWA wiki iliyopita kuwa bei kikomo ya nishati, ambayo inashughulikia idadi kubwa ya kaya za huko Uingereza, ingepanda kwa asilimia 80% hadi jumla ya wastani ya kila mwaka ya Euro £3,549 kutoka Oktoba.
Liz Truss ataweka mpango wake siku ya Alhamisi wa kusaidia kaya na biashara na gharama zinazoongezeka za nishati.
Downing Street ilisema hatua hiyo itakuwa “ya ujasiri” na “maamuzi” na itasaidia watu kote Uingereza wanaokabiliwa na bili kubwa za nishati, na pia kuongeza usambazaji wa nishati ya ndani.
Bi Truss anatarajiwa kufichua mapendekezo yake kwa Bunge, na kufungua mjadala wa jumla kuhusu gharama za nishati.

Baada ya miezi kadhaa ya ukosoaji juu ya ukosefu wa usaidizi wa ziada wa kudhibiti athari za mfumuko wa bei unaotokana na ukubwa wa bei ya nishati, ambao umefikia kiwango cha juu cha miaka 40, mpango wa Bi Truss wa kukabiliana na gharama ya maisha utakuwa mpango wa kwanza mkuu wa sera zake za uwaziri mkuu .
Dalili za mapema zinaonyesha kusimamishwa kwa bei kunakuja – na Hazina inaweza kuzilinda familia kabisa dhidi ya kulipia gharama kubwa kununua nishati.
Anatarajiwa kufungia bili za kaya kwa takriban pauni 2,500, lakini amekataa wazo la kutumia ushuru wa ziada kwaua utafaidisha zaidi makampuni makubwa ya mafuta na gesi kufadhili kifurushi hicho – kilichoripotiwa kugharimu hadi £150bn.
Bili zinaweza kurudi kwenye kiwango cha sasa cha takriban Euro £2,000 mara tu ruzuku ya Euro £400 kwa kila kaya na marekebisho mengine ya bili yanatekkelezwa kkatika mpango huo wa Bi Truss wakupunguza bei ya nishati Uingereza.
Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.