×

Rais Samia Ahutubia Kwenye Maadhimisho ya Miaka 10 ya Chuo cha NDC, Kunduchi Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wageni mbalimbali kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) yaliyofanyika Chuoni hapo Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan amehutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC), Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Rais  Samia akikabidhiwa Cheti kama ishara ya kutunukiwa Tuzo ya Heshima ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) na Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo hicho Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.
Rais  Samia  akipewa Tuzo ya Heshima ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax.
Matukio mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) yaliyofanyika Chuoni hapo Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.

Leave a Comment